Aliyekuwa mbunge wa Tetu akamatwa ▷ Kenya News

Aliyekuwa mbunge wa Tetu akamatwa ▷ Kenya News

Aliyekuwa mbunge wa Tetu Ndung’u Gethenji amekamatwa na makachero jijini Nairobi.

Kulingana na gazeti la Nation, mwanasiasa huyo alitiwa mbaroni na maafisa kutoka kitengo cha Flying Squad Ijumaa, Oktoba 18.

Habari Nyingine: Akaunti feki za viongozi zawavunja mbavu Wakenya mitandaoni

Aliyekuwa mbunge wa Tetu akamatwa

Mbunge wa Tetu Ndung’u Gethenji alikamatwa jijini Nairobi Ijumaa Oktoba18. Picha: Nation
Source: Facebook

Haijabainika kilichofanya Ndung’u kutiwa mbaroni lakini kumekuwa na mvutano kati yake na nduguye kuhusu mali iliyo jijini Nairobi.

Duru zinaarifu kuwa wawili hao wanazozana kuhusu umiliki wa nyumba zilizo kwenye mtaa wa kifahari wa Kitsuru jijini Narobi.

Mengi kufuata …

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia news@tuko.co.ke au WhatsApp: 0732482690.

Subscribe to watch new videos

administrator

Related Articles