Arsene Wenger sasa anataka kuwa kocha wa Man United ▷ Kenya News

Arsene Wenger sasa anataka kuwa kocha wa Man United ▷ Kenya News

– Arsene Wenger alikuwa meneja wa Arsenal kwa miaka 22

– Kocha huyo alishinda mataji 10 wakati wa uongozi wake

– Wenger mwenye umri wa miaka 69 kwa sasa ameweka wazi nia yake ya kutaka kuwanoa Man United

Aliyekuwa kocha wa Arsenal, Arsene Wenger, amekiri kuwa itakuwa furaha kubwa kwake kuwa meneja wa Manchester United.

Wenger hajakuwa uwanjani tangu kutengana na Gunners mwaka 2018, baada ya kumaliza miaka 22 ya utawala wake katika klabu hiyo ya London.

Habari Nyingine: EFL CUP: Chelsea kumenyana na Man United, Arsenal wakialikwa na Liverpool

Arsene Wenger sasa anataka kuwa kocha wa Man United

Arsene Wenger, amekiri kuwa itakuwa furaha kubwa kwake kuwa meneja wa Manchester United.
Source: Getty Images

Habari Nyingine: EFL Cup: Chelsea wafufua ushindi wao, wapepeta Grimsby Town 7-1

Mwaka wake wa mwisho Arsenal ulikumbwa na masaibu tele, huku mashabiki wakifanya maisha yake kuwa magumu kwa kumtaka ajiuzulu.

Hata hivyo, Mfaransa huyo anadai kuwa na nguvu na uwezo wa kuiongoza Man United, na pia kudokezea ana mapendekezo kadhaa ya jinsi ya kuinoa timu hiyo.

Habari Nyingine: Afya Yako: Fahamu faida 7 za kunywa maji la limao

“Kuwa meneja wa Manchester United ni ndoto ya kila kocha. Meneja yeyote mwenye nguvu na uwezo anaweza kuiongoza,” Wenger aliambi beIN Sports.

Mashetani Wekundu walianza msimu mpya kwa vishindo, kwa kuandikisha ushindi mara mbili katika mechi sita walioshiriki na kuridhika katika nafasi ya nane kwenye jedwali ya Ligi Kuu.

Habari Nyingine: Mwanga wa Kiswahili: Utata wa vitate sehemu ya pili

Kikosi hicho kinachofunzwa na Ole Gunnar Solskjaer kilijipatia ushindi kupitia mikwaju ya penalti dhidi ya timu ya League One, Rochdale katika mashindano ya Kombe la EFL.

Lakini Wenger anaamini kuwa timu hiyo ina wachezaji mahiri ila ukosefu wa mafunzo kamili ya mazoezi ndio kizingiti ya kurejesha ubingwa wao.

“Timu hiyo inakosa mfumo wa kucheza na kujiimarisha. Kuna timu hapo, lakini inatakiwa kuongozwa na kuelekezwa,” alitambua kocha huyo.

Wenger, alipoulizwa endapo angependelea kutwaa kiti hicho Old Trafford, hakuficha nia yake.

“Kama nilivyosema, kufanya kazi Manchester United ni kama ndoto kutimia kwa kocha yeyote. Niko na ujasiri….na niko sawa,” alikiri kocha huyo.

READ ENGLISH VERSION

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia news@tuko.co.ke au WhatsApp: 0732482690.

Subscribe to watch new videos

administrator

Related Articles