Bwana harusi aliyetoweka na kisha kupatikana asema mipango ya harusi bado ipo ▷ Kenya News

Bwana harusi aliyetoweka na kisha kupatikana asema mipango ya harusi bado ipo ▷ Kenya News

Bwana harusi aliyeripotiwa kutoweka kaunti ya Taita Taveta na kisha kupatikana miezi miwili kabla ya harusi yake ameihakikishia familia yake pamoja na marafiki kuwa harusi bado ipo.

James Mwamburi ambaye alitoweka kwa siku kadhaa alipatikana Jumatano, Oktoba 16 baada ya kutafutwa kwa kina na jamaa wake wakishirikiana na maafisa wa polisi.

Habari Nyingine: Nakuru: Pasta mpenda pesa abaki bila waumini

Kama ilivyoripotiwa awali na TUKO.co.ke, Mwamburi alitekwa nyara na watu wasiojulikana Jumatatu Oktoba 7.

Kwa mujibu wa taarifa za KTN News, Mwamburi alipatikana karibu na eneo la Man Eaters katika barabara ya Mbololo akiwa amefungwa miguu na mikono.

Habari Nyingine: Jombi aangua kilio unga kupotea njiani

Bwana harusi aliyetoweka na kisha kupatikana asema mipango ya harusi bado ipo

Mwamburi alitekwa nyara na watu wasiojulikana Jumatatu Oktoba 7.
Source: Original

Familia yake ilimpeleka katika hospitali ya Voi ambapo alifanyiwa ukaguzi wa kimatibabu kabla ya kuruhusiwa kwenda nyumbani.

Aidha, Mwamburi ambaye anatarajiwa kufunga pingu za maisha na kipenzi chake cha Roho Dorcas Wairimu alisema mipango ya harusi ingali ipo na itafanyika mwezi Desemba.

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia news@tuko.co.ke au WhatsApp: 0732482690.

Tazama habari zaidi kutoka TUKO.co.ke

Subscribe to watch new videos

administrator

Related Articles