Chelsea vs Lille: Blues warejesha makali yao ugenini wacharaza wenyeji 2-1 ▷ Kenya News

Chelsea vs Lille: Blues warejesha makali yao ugenini wacharaza wenyeji 2-1 ▷ Kenya News

– Mechi kati ya Lille na Chelsea ilitamatika 2-1 kwa faida ya Blues

– Abraham na Willian walifunga bao kila mmoja na kuipatia Chelsea ushindi

– Victor Osimhen alifungia Lille bao la kufutia machozi katika kipundi cha kwanza

Mchezaji kinda wa Chelsea, Tammy Abraham, mnamo Jumatano, Oktoba 2 usiku, aliendeleza uledi wake baada ya kuisaidia Chelsea kutwaa ushindi wa 2-1 dhidi ya Lille katika mechi ya Klabu Bingwa Ulaya, ugani Stade Pierre-Mauroy.

Chelsea walikuwa kwenye harakati ya kurejesha makali yao kwenye kampeni yao baada ya kunyukwa 1-0 na Valencia katika mechi yao ya ufunguzi ya Kundi H uwanjani Stamford Bridge.

Habari Nyingine: Sportpesa yawafuta kazi wafanyakazi wake 400 baada ya kusitisha biashara yake Kenya

Habari Nyingine: Tottenham waadhibiwa vikali na Bayen Munich, nyumbani

Frank Lampard alikuwa ameimarisha kikosi chake kilichosafiri Ufaransa, akiwa na matumaini kuwa ushindi ugenini ulitosha kufufua uledi wao Uropa.

N’Golo Kante, ambaye alikuwa na kumbana na kuwa fiti alishirikishwa katika awamu ya kwanza, baada ya kukosa mechi ya Jumamosi iliyopita ya Ligi Kuu dhidi ya Brighton kwa sababu ya kuuguza jeraha la mguu.

Habari Nyingine: IAAF 2019: Ferguson Rotich ajishindia medali ya shaba katika mbio za mita 800

Abraham kwa mara nyingine tena alikabithiwa nafasi ya kuongoza safu hiyo, huku chipukizi huyo akimthibitishia Lampard imani kwake kwa kufungua ukurasa wa mabao kunako dakika ya 22.

Fowadi huyo alichonga ndizi hadi kimyani akiwa karibu na lango ya wenyeji na kutingisa wavu.

Habari Nyingine: Nyota wa mchezo wa miereka The Rock, atangaza kurejea WWE

Lakini Victor Osimhen aliwafungia wenyeji dakika 10 baadaye, huku nyota huyo wa Nigeria akifunga kupitia kona.

Huku awamu ya kwanza ikitamatika kwa 1-1, upande zote mbili zilianza mashambulizi katika kipundi cha pili, vilabu vyote vikitafuta ushindi.

Hata hivyo, wageni ndio walirejesha ushindi wao kupitia kwa kijana Willian ambaye alitumia vizuri pasi aliyochongewa na Callum Hudson-Odoi na kuwasaidia Blues kutwaa ushindi wa 2-1 katika mechi yake ya 30 na klabu hiyo.

Kwa sasa wenyeji hao wa Stamford Bridge wameridhika katika nafasi ya pili kundini H, nyuma ya viongozi Ajax.

READ ENGLISH VERSION

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia news@tuko.co.ke au WhatsApp: 0732482690.

Subscribe to watch new videos

administrator

Related Articles