Gavana Anne Mumbi adai Aukot ana kiburi ▷ Kenya News

Gavana Anne Mumbi adai Aukot ana kiburi ▷ Kenya News

– Mabunge 31 kati ya 47 yameuangusha mswada wa Punguza Mizigo

– Wawakilishi wadi walisema sababu kuu ya kuupiga teke mswada huo ni kwa kuwa unadhalilisha haki za uongozi wa wanawake

– Gavana Anne Mumbi amedai mswada huo ulionesha dalili za kufeli kwa kuwa Ekuru alikuwa na kiburi

Gavana wa Kirinyaga Anne Mumbi amemshambulia kiongozi wa Chama cha Thirdway Alliance Ekuru Aukot, baada ya mswada wake wa Punguza Mizigo kupigwa teke na kaunti 24 kati ya 47.

Julai 2019, IEBC ilitangaza kuwa Aukot alikuwa amefaulu kusanya takriban saini milioni moja kutoka kwa Wakenya na hivyo basi kuupa nafasi mswada wake kujadiliwa katika majimbo yote 47.

Habari Nyingine: Wanasiasa wa Kieleweke washangilia kuanguka kwa Punguza Mzigo

Gavana Anne Mumbi adai Aukot ana kiburi

Picah ya wali ya Ekuru Aukot. Gavana Anne Mumbi amedai kiongozi huyo ana kiburi. Picha: Ekuru Aukot
Source: Facebook

Hata hivyo, mswada huo ulipata pigo Jumatano, Oktoba 16, baada ya mabunge 31 kati ya 47 kuupiga teke kumaanisha kuwa hauwezi kujadiliwa katika bunge la kitaifa.

Wawakilishi wa maeneo bunge katika kaunti walisema sababu kuu ya kuuangusha mswada huo ni kwa kuwa unadhalilisha haki za wanawake na kuwanyima fursa ya kuwa viongozi.

Miongoni mwa mapendekezo ya mswada huo ni kupunguza idadi ya wabunge hadi 147.

Habari Nyingine: Tony Gachoka amrarua Muroken mzimamzima baada ya kuachiliwa huru kutoka seli

Kufuatia tukio hilo, gavana wa Kirinyaga Anne Mumbi amesema kuwa mswada wa Aukot ulionesha dalili za kuanguka kwani alikuwa mwingi wa kiburi hakutilia maanani ushauri wa watu jinsi K24 ilivyoripoti.

Gavana Anne Mumbi adai Aukot ana kiburi

Gavana Anne Mumbi akiwahutubia waandishi wa habari. Picha: K24 Digital
Source: Depositphotos

“Aukot ni mtu wa kiburi ambaye aliamua kushika njia yake pekee na kupuuza hisia za Wakenya,” gavana huyo alisema katika hotuba yake kwa waandishi wa habari Alhamisi, Oktoba 17.

Majimbo yaliyoutupa nje mswada wa Aukot ni Kajiado, Nyandarua, Kilifi, Trans-Nzoia, Garissa, Nandi, Elgeyo-Marakwet, Kericho, Kisumu, Meru, Tana River, Busia, Nairobi, Kiambu, Siaya, Nakuru, Murang’a, Kakamega, Kisii, Kirinyaga, Nyamira, Makueni, Nyeri, Mandera, Lamu, na Homa Bay.

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia news@tuko.co.ke au WhatsApp: 0732482690.

administrator

Related Articles