Jacque Maribe awasha moto mtandaoni baada ya kufichua baba wa mtoto wake ▷ Kenya News

Jacque Maribe awasha moto mtandaoni baada ya kufichua baba wa mtoto wake ▷ Kenya News

Aliyekuwa mwanahabari wa runinga ya Citizen Jacque Maribe Alhamisi, Oktoba 17, aliwasha moto kwenye mtandao baada ya kufichua baba wa mtoto wake kwa mara ya kwanza.

Jacque alifichua hayo kupitia kwa picha aliyochapisha kwenye mtandao wake baada ya kusherekea siku ya kufuzu kwa mwanawe huyo anayejulikana kama Zahara.

Habari Nyingine: Wanasiasa wa Kieleweke washangilia kuanguka kwa Punguza Mzigo

Jacque Maribe awasha moto mtandaoni baada ya kufichua baba wa mtoto wake

Mwanahabari Jacque Maribe hatimaye amefichua baba ya mtoto wake Zahari. Picha: UGC
Source: Instagram

Kwenye picha hiyo, Maribe alifiichua kuwa baba ya Zahari si mwingine mbali mchekeshaji Eric Omondi.

Wawili hao waliamua kuchapisha picha za mtoto wao kwa pamoja kwenye kurasa zao za Instagram.

Habari Nyingine: Tony Gachoka amrarua Muroken mzimamzima baada ya kuachiliwa huru kutoka seli

Jacque Maribe awasha moto mtandaoni baada ya kufichua baba wa mtoto wake

Jacque Maribe aliwasha moto mtandaoni baada ya kufichua baba wa mtoto wake. Picha: UGC
Source: Instagram

Kina paparazi mjini wamekuwa wakijaribu kupekua ni nani baba wa mtoto huyo bila kufaulu ingawa kumekuwa na uvumi kuwa wawili hao walikuwa na uhusiano.

Hata hivyo, mwanablogu Dennis Itumbi ndiye amekuwa akiangaziwa sana na kudaiwa kuwa huwa anamuwinda Maribe kutokana na urafiki wao wa karibu.

Itumbi aliwapongeza wawili hao baada ya kuamua kujitokeza na kukiri kuwa walijaliwa mtoto pamoja.

Habari Nyingine: Matokeo ya upasuaji wa miili ya Mariam na mwanawe kutolewa na taarifa zingine

“Familia kwanza. Siku njema wakati wa kufuzu kwako, mama na baba Eric Omondi tunajivunia wewe!” Maribe alisema.

Maisha ya Maribe kimapenzi yalikuwa kwenye umma wakati ambapo Jowie Irungu alimuomba penzi hadharani.

READ ENGLISH VERSION

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia news@tuko.co.ke au WhatsApp: 0732482690.

Subscribe to watch new videos

administrator

Related Articles