Jose Mourinho aibuka kuwa chaguo bora kumrithi Mauricio Pochettino kama kocha wa Tottenham ▷ Kenya News

Jose Mourinho aibuka kuwa chaguo bora kumrithi Mauricio Pochettino kama kocha wa Tottenham ▷ Kenya News

– Jose Mourinho ameibuka kuwa chaguo bora ya kuwa meneja mpya wa Tottenham

– Klabu hiyo ya Ligi Kuu imekuwa ikikumbwa na wakati mgumu baada ya kuandikisha matokeo mabovu msimu huu

– Aliyekuwa kocha wa Juventus, Massimilliano Allegri pia amehusishwa na kuteuliwa kocha wa Spurs

Jose Mourinho ameibuka kuwa chaguo bora wa kumrithi Mauricio Pochettino kama meneja wa Tottenham.

Raia huyo wa Argentina amekuwa motoni wiki hii baada ya Spurs kubanduliwa kwenye kinyang’anyiro cha Kombe la Carabao na mahasidi wao w jadi Colchester United.

Habari Nyingine: Sportpesa yawafuta kazi wafanyakazi wake 400 baada ya kusitisha biashara yake Kenya

Habari Nyingine: Wachezaji wa AFC Leopards wagoma kulalamikia malimbikizo ya mishahara yao

Kichapo hicho kilifuatwa na adhabu nyingine kali ya 7-2 kutoka kwa Bayern Munich katika mechi ya Klabu Bingwa Ulaya mnamo Jumanne, Oktoba 1.

Kwa mujibu wa SportNation.be, Mourinho ndiye mgombea wa kwanza anayeng’ang’ania nafasi hiyo ya Pochettino.

Pochettino ni miongoni mwa makocha sita wa Ligi Kuu sita ambao wana uwezekano mkubwa wa kupigwa kalamu.

Habari Nyingine: Chelsea vs Lille: Blues warejesha makali yao ugenini wacharaza wenyeji 2-1

Hata hivyo, Mourinho anapigiwa upato ya kuwa meneja wa Tottenham kwa uwezekano wa 3/1.

Aliyekuwa kocha wa zamani wa Juventus, Max Allegri anatazamiwa pia kuchukua wadhifa huo kwa uwezekano wa 5/1 naye Eddie Howe wa Bournemouth akiwa na 6/1 kumpokonya Pochettino kazi hiyo.

Licha ya Mourinho kufuzu katika taaluma yake nchini Ureno, Uingereza, Italia na Uhispania, alitimuliwa ugani Old Trafford mwezi Desemba mwaka jana.

Mreno huyo ambaye hajakuwa uwanjani kwa muda, kwa sasa anahudumu kama mtaalam wa michezo.

READ ENGLISH VERSION

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia news@tuko.co.ke au WhatsApp: 0732482690.

Subscribe to watch new videos

administrator

Related Articles