Korti yamruhusu askofu kuvunja ndoa yake ya miaka 21 kwa kunyimwa tendo la ndoa ▷ Kenya News

Korti yamruhusu askofu kuvunja ndoa yake ya miaka 21 kwa kunyimwa tendo la ndoa ▷ Kenya News

Mahakama imeamua ndoa ya miaka 21 kati ya askofu mmoja jijini Mombasa na mkewe kutamatika kwa madai ya kunyimwa haki ya ndoa na uzinzi.

Mnamo Ijumaa , Septemba 20, Hakimu Mkaazi Joshua Nyariki alimruhusu Askofu Evans Mayenyo Elegwa na Pasta Hellen Jalenga Luyali kutalakiana kwani ndoa yao ilikuwa imezingirwa na utata.

Habari Nyingine: Pierre-Emerick Aubameyang aisaidia Arsenal kuilima Aston Villa 3-2 bila huruma

Mahakama

Askofu Evans Mayenyo Elegwa na Pasta Hellen Jalenga Luyali walikuwa kwenye ndoa ya miak 21.
Source: Facebook

Habari Nyingine: Pasta Nga’ng’a kuwazaba makofi waumini wake na habari zingine zilizotamba sana

“Haitakuwa haki mimi kuwaruhusu wawili hawa kuendelea kuishi pamoja katika ndoa iliyozingiriwa na utata na hakuna aliyetayari kumsamehe mwenzake,” aliamuru hakimu Nyariki.

Askofu Elegwa alifungua kesi ya talaka huku mkewe akifikika mahakamani kuwasilisha kesi ya kutaka kugawana mali ambapo kesi hiyo ilikataliwa.

Habari Nyingine: Manchester United waadhibiwa 2-0 na West Ham

Kwa mujibu wa Standard, wawili hao walifunga pingu za maisha mwaka wa 1995, na kujaliwa watoto watatu ambao kwa sasa wana umri wa miaka 23 na 19 na pia kuasili watoto wengine wawili wa kati ya umri wa miaka 25 na 19.

Katika malalamishi yake, Elegwa ambaye ni mhubiri wa kanisa ya Bahari Pentecostal, jijini Mombasa, aliambia mahakama kuwa mkewe aliondoka nyumbani kwao mwaka 2016 na kukataa kurudi.

Korti yamruhusu askofu kuvunja ndoa yake ya miaka 21 kwa kunyimwa tendo la ndoa

Elegwa aliambia mahakama kuwa mkewe aliondoka nyumbani kwao mwaka 2016 na kukataa kurudi.
Source: Facebook

Habari Nyingine: Dadake bilionea Tob Cohen aondoka nchini kabla ya mazishi kufanyika

Akitoa uamuzi wake siku ya Ijumaa, hakimu alisema kwamba aliridhika na ushahidi uliotolewa na mhubiri huyo kuwa ndoa yao ilikuwa imevunjika.

Hata hivyo, Luyali alipuzilia mbali madai ya mumewe kwa kudai kuwa alifukuzwa nyumbani kwao mwaka 2016 baada ya mumewe kurejea nchini kutoka Singapore.

Liyali pia alipinga madai ya Elegwa kuwa alijaribu kumzungumzia ili wapate kurudiana.

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia news@tuko.co.ke au WhatsApp: 0732482690.

Subscribe to watch new videos

administrator

Related Articles