Magazeti ya Kenya Alhamisi, Septemba 26: Babu wa miaka 90 apashwa tohara kabla ya kuzikwa ▷ Kenya News

Magazeti ya Kenya Alhamisi, Septemba 26: Babu wa miaka 90 apashwa tohara kabla ya kuzikwa ▷ Kenya News

Shinikizo la kinara wa upinzani Raila Odinga kutaka kuwa na mfumo wa serikali ya bunge na mkutano wa Rais Uhuru Kenyatta na mwenzake wa Somalia Mohamed Farmajo ndizo taarifa zilizopewa uzito katika magazeti ya Alhamisi, Septemba 26.

Magazeti haya pia yameangazia hatua ya Waziri wa Elimu George Magoha kufunga shule moja jijini Naorobi kwa sababu za usalama.

1. People Daily

Katika gazeti hili hatua ya Gavana wa Nairobi Mike Sonko kuwafurusha maafisa 16 wa kaunti umeelezewa kama mpango wake wa kurejesha na umma.

Hata hivyo, jambo ambalo limewashangaza wengi ni kumrejesha aliyekuwa naibu mwenyekiti wa bodi ya uchaguzi katika Chama cha Jubilee na pia mwandani wa Naibu Rais William Ruto, Veska Kangogo.

Awali Sonko alikuwa amemtimuwa Kangogo kwa madai ya kusafiri nchini Marekani bila ya idhini yake lakini kurejeshwa ofisini baadaye.

Pia imeibuka kuwa Kangogo alikuwa kwenye orodha ya aibu ya Rais Uhuru ambayo iliwasilishwa bungeni mwaka 2016, kwa kuhusika kwenye sakata ya NSSF lakini aliweza kuondolewa lawama.

2. Taifa Leo

Gazeti hili linaripoti kuhusu kisa cha kutamausha killichotokea Kaunti ya Muranga ambapo maiti ilipashwa tohara kabla ya kuzikwa.

Jamaa wa mzee mwenye umri wa miaka 90, Erastus Githinji, ilitambua kwamba mwenzao hakuwa amepashwa tohara wakati walikuwa wakimvalisha nguo katika chumba cha maiti cha Maragua.

Mkutano wa dharura uliandaliwa na wazee kukubaliana kuwa lazima matambiko maalum yangefanywa kabla ya mzee huyo kuzikwa.

Kulingana na wazee hao, ilikuwa aibu na kinyume cha tamaduni kwa mwanamume aliyekuwa na mke wa miaka 72 , watoto na wajukuu kuzikwa bila kupitia kisu cha ngariba.

Mkewe alitozwa faini ya mbuzi watatu, na pombe ya kitamaduni baada ya wazee kumkashifu kwa kukosa kuwafahamisha habari hizo kwa miaka 56 waliyoishi pamoja.

Hata hiyo, mama huyo aliwalaumu marafiki zake wa karibu na ngugu zake kwa kudai kuwa ilikuwa jukumu lao kumzuia mumewe kwa aibu.

3. The Star

Kando na tamaduni ya kawaida ambapo watu wengi hupendelea kuzikwa ama mwili wao kuchomwa, mwanamume mmoja kutoka Gatundu Kusini amewashangaza wengi katika kijiji chake kwa kutangaza kuwa mwili wake hautazikwa atakapofariki.

Katika uradhi wake wa mwisho, John Kihiu Nduku anataka mwili wake kutumiwa katika masamo ya mwili wa binadamu katika Chuo Kikuu cha Jomo Kenyatta.

Nduku alisema alifanya uhamuzi huo kutokana na hali yake ya kimatibabu ambapo amekuwa akiuuga kwa miaka 29 lakini kufaulu kutibiwa mwaka huu.

“Nilikuwa na furaha sana. Nimekuwa na maumivu sana na njia moja tu ya kutoa shukrani zangu ni kwa kuwasaidia wanafunzi wanaosomea udaktari kwa kuwapea mwili wangu,”

“Nimekuwa nikitembelea hospitali mbali mbali kila mara tangu mwaka 1990 wakati matatizo haya yalianza. Ni mwezi Februari tu ndipo madaktari wa Gatundu walitambua ugonjwa niliyokuwa nikiugua,” alisema Nduku.

administrator

Related Articles