Mama aunganishwa na mwanawe aliyedhania alifariki dunia miaka 30 iliyopita ▷ Kenya News

Mama aunganishwa na mwanawe aliyedhania alifariki dunia miaka 30 iliyopita ▷ Kenya News

Ilikuwa furaha tele baada ya mama kuunganishwa na mwanawe aliyedhania alifariki dunia miaka 30 iliyopita wakati alipozaliwa

Tina Bejarano ambaye ni raia wa Marekani alijaliwa mtoto msichana aliyempatia jina la Kristin Cooke ila akaambiwa baadaye na mamake mzazi kuwa mtoto huyo alifariki dakika 15 tu baada ya kuzaliwa.

Habari Nyingine: Jombi aangua kilio unga kupotea njiani

Mama aunganishwa na mwanawe aliyedhania alifariki dunia miaka 30 iliyopita

Mama aunganishwa na mwanawe aliyedhania alifariki dunia miaka 30 iliyopita
Source: UGC

Habari Nyingine: Oscar Sudi amtaka Atwoli kukoma kuwanyemelea mabinti za watu

Iligunduliwa baadaye kuwa mamake Tina alipanga njama ya kumtwaa mtoto huyo kwa madai kuwa Tina alikuwa msichana mdogo mwenye umri wa miaka 17 pekee na hangeweza kuyakimu maisha yake pamoja na ya mtoto.

Mtoto huyo alienda kuishi na wazazi wake walezi mjini Les Vegas hadi Tina alipopokea ujumbe kwenye barua pepe hivi majuzi kwamba wazazi hao wangeendelea kumlea.

Vipimo vya DNA vilifanywa na ikabainika kuwa ni mwanawe ila la kushangaza Kristin ni mwanaume kwa sasa kwani alibadilisha jinsia yake na pia ameoa.

Habari Nyingine: Nakuru: Pasta mpenda pesa abaki bila waumini

Hata hivyo, Tina alisema sio hoja kwake kwa Kristin kubadilisha jinsia kwani ni mwanawe na anafurahia kwamba yuko hai.

” Sijali hata kama alibadilisha jinsia, sijali hata kidogo, huyu ni mwanangu, nashukuru yu hai,”Tina alisema.

Read: ENGLISH VERSION

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia news@tuko.co.ke au WhatsApp: 0732482690.

Tazama habari zaidi kutoka TUKO.co.ke

Subscribe to watch new videos

administrator

Related Articles