Mama jasiri aliyesusia matibabu ya saratani kumuokoa mwanawe tumboni afariki ▷ Kenya News

Mama jasiri aliyesusia matibabu ya saratani kumuokoa mwanawe tumboni afariki ▷ Kenya News

TUKO.co.ke inasikitika kutangaza kifo cha Anne Ameyo, mwanamke mwenye ujasiri kutoka jijini Nairobi ambaye alikataa kufanyiwa matibabu ya saratani kumuokoa mwanawe aliyekuwa tumboni.

Anne alifariki Jumapili, Septemba 22, akipokea matibabu katika hospitali ya Glen Eagles Global huko India.

Habari Nyingine: Msanii Jose Chameleone ahamisha familia yake Marekani dhidi ya siasa chafu za Uganda

Mama jasiri aliyekataa matibabu ya saratani kuwaokoa wanawe tumboni aaga dunia

Anne aliwagusa wengi mioyo baada ya kususia matibabu ya saratani ili kuokoa maisha ya mwanawe aliyekuwa tumboni. Picha: TUKO.co.ke/ Edwin Ochieng’
Source: Original

Akizungumza na mtangazaji wa TUKO.co.ke Lynn Ngugi, mamake Anne, Jane Muchuka Ameyo alisema kuwa kifo cha mwanawe kimeiacha familia yake na majonzi yasiyoelezeka.

Alifichua kuwa, maneno ya mwanawe ya mwisho kabla ya kukata roho yalikuwa ni ‘Mungu usiniache.”

Habari Nyingine: Magazeti ya Kenya Jumanne, Septemba 24: Dadake Tob Cohen afichua ni kwa nini hatohodhuria mazishi ya kakake

Vile vile Ameyo aliwashukuru Wakenya kwa kumchangia takriban KSh 2.3 milioni, fedha ambazo ziligharamia nauli yake na matibabu hospitalini India.

Mama jasiri aliyekataa matibabu ya saratani kuwaokoa wanawe tumboni aaga dunia

Anne alifariki akiwa India akipokea matibabu ya saratani. Picha: TUKO.co.ke/Edwin Ochieng’
Source: Original

Kulingana na mzazi huyo, Anne alikuwa mwingi wa furaha na alikuwa tayari kabisa kurejea nyumbani kabla ya kifo chake kutokea ghafla.

Anne aliwaomba Wakenya kumchangia KSh 180,000, fedha ambazo alihitaji kutumia kama nauli kurejea nyumbani.

TUKO.co.ke ilibaini kuwa Anne aliwasili India Agosti 15 na kuanza kupokea matibabu kabla ya kupoteza maisha yake ghafla.

Habari Nyingine: Mama atiwa nguvuni kwa kutumia unga wa chakula cha nguruwe kuokea watu mikate

Marehemu amewaacha watoto wawili ambao kulingana na mamake anahitaji msaada ili kuwalea hususan baada ya kifo cha mama yao.

TUKO.co.ke iliangazia taarifa ya Anne mapema Julai 2019 ambapo alionesha ujasiri mwingi na matumaini ya kupona.

Mama jasiri aliyekataa matibabu ya saratani kuwaokoa wanawe tumboni aaga dunia

Mama mwenye ujasiri aliyekataa matibabu ya saratani kuwaokoa wanawe tumboni aaga dunia. Picha: UGC
Source: UGC

Anne aliwaguza wengi mioyo kwa kususia matibabu ya saratani ili kuyaokoa maisha ya mwanawe aliyekuwa tumboni.

“Nimepitia mengi sana tangu 2017. Nilipatikana na maradhi ya saratani. Madaktari walinishauri nichague kuavya mimba mwanangu afe au mimi nitafariki iwapo mtoto huyo atazaliwa,” alifichua wakati wa mahojiano na TUKO.co.ke

Habari Nyingine: Mwea: Shambaboi amwaga unga alipofumaniwa na mwajiri akimpapasa mpishi

“Nilikataa kuavya maimba ya mwanangu na kuwaarifu kwamba Mungu alikuwa na sababu ya kunipa mtoto huyo,” aliongeza.

Kufuatia kifo chake, Wakenya walifurika katika mitandao ya jamii kutuma rambi rambi zao kwa familia ya marehemu.

Read ENGLISH VERSION

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia news@tuko.co.ke au WhatsApp: 0732482690.

Subscribe to watch new videos

administrator

Related Articles