Mwanabodaboda amfumania binamuye akifungua ‘server’ za mkewe mwenye mimba ya miezi 8 ▷ Kenya News

Mwanabodaboda amfumania binamuye akifungua ‘server’ za mkewe mwenye mimba ya miezi 8 ▷ Kenya News

Wakazi wa kijiji cha Nyakunguru kaunti ya Nyamira walishuhudia sinema ya bure Alhamisi, Octoba 3, baada ya mhudumu wa bodaboda kumfumania mkewe ambaye ni mja mzito akila uroda na binamuye.

Kando na wawili hao kuwa wa jamii moja, majamaa hao ambao wana umri wa makamo ni marafiki wa dhati ambao mara kwa mara huonekana pamoja.

Habari Nyingine: Sonko awataka wanyikazi wa kaunti kuvaa suti

Mwanabodaboda amfumania binamuye akifungua 'server' za mkewe mwenye mimba ya miezi 8

Mama huyo wa mtoto mmoja ana uja uzito wa mtoto wa pili. Picha: UGC
Source: UGC

Hata hivyo, kijogoo huyo ambaye anatambulika kama Basweti anasemekana kummezea mate mkewe Job, na kupeleka wawili hao kuanza uhusiano wa mapenzi ambao umekuwa ukiendelea kwa miezi.

Job alinong’onezewa na majirani kuhusu uhusiano wa mapenzi ambao ulikuwa unaendelea baina ya mkewe na binamuye.

Alipomuuliza mkewe kuhusu fununu hizo, mama alijitetea vikali na kusema kuwa hawezi akafanya mapenzi na mume mwingine ilhali alikuwa mja mzito tayari.

Job aliamua kufanya uchunguzi zaidi hadi Alhamisi alipowafumania wawili hao kitandani siku zao za arobaini zilipowadia.

Habari Nyingine: Precious Talent: Gavana Sonko atishia kuwatimua wafanyikazi wa kaunti waliofyonza hela za waathiriwa

Mwanabodaboda amfumania binamuye akifungua 'server' za mkewe mwenye mimba ya miezi 8

Job ambaye ni mhudumu wa bodaboda kaunti ya Nyamira alipashwa na majirani kuwa mkewe alikuwa anachumbiana na binamuye. Picha: UGC
Source: UGC

Siku hiyo, Job aliingia katika chumba chao cha kulala kupitia dirisha na kuwafumania binamuye na mkewe kitandani mwake.

Job alitoka nje akipiga mayowe kuwaita majirani huku binamuye ambaye alihofia kichapo akihepa mara moja.

Habari Nyingine: Vyakula na vinywaji kutoka nje vyapigwa marufuku SGR

“Job hajakuwa akienda kazini kwa siku tatu tangu alipopata habari kwamba binamuye alikuwa anahusiana kimapenzi na mkewe,” jirani mmoja ambaye hakutaka kutajwa aliiambia TUKO.co.ke.

“Huenda mtu alimuarifu Job kupitia kwa njia ya simu kwamba Basweti ameonekana akiingia bomani mwake,” jirani huyo alisema.

Subscribe to watch new videos

administrator

Related Articles