Nitasafirisha miili ya Mariam Kigenda na Amanda hadi Makueni – Sonko ▷ Kenya News

Nitasafirisha miili ya Mariam Kigenda na Amanda hadi Makueni – Sonko ▷ Kenya News

– Sonko alisema atagharamia usafiirishaji wa miili ya Mariam na mwanawe Amanda

– Wawili hao watasafirishwa kutoka Mombasa hadi Makueni kisha kuzikwa Jumamosi, Oktoba 19.

– Mariam na Amanda walifariki baada ya kuishiwa na pumzi wakiwa baharini

– Kufauatia mkasa huo rais Uhuru amemfuta kazi mwenyekiti wa KFS Dan Mwazo na bodi yake nzima

Gavana wa Nairobi Mike Sonko amesema kuwa ataisafirisha miili ya waathiriwa wa mkasa wa Likoni Mariam Kigenda na mwanawe Amanda Mutheu kutoka Mombasa hadi Makueni.

Msemaji wa familia ya Kigenda Luka Mbaati alisema, miili ya wawili hao itasasafirishwa kutoka chumba cha kuhifadhi maiti cha Jocham kaunti ya Mombasa Ijumaa, Oktoba 18.

Habari Nyingine: Gavana Anne Mumbi adai Aukot ana kiburi

Nitasafirisha miili ya Mariam Kigenda na Amanda hadi Makueni - Sonko

Gavana Mike Sonko amesema ataisafrisha miili ya waathiriwa wa mkswa wa Likoni kutoka Mombasa hadi Makueni. Picha: Mike Sonko
Source: Facebook

Kwa mujibu K24 Digital, Sonko alifichua kuwa ataisafirisha miili hiyo bila malipo hadi eneo bunge la Kilome, kaunti ya Makueni kwa ajili ya mazishi yao ya Jumamosi, Oktoba 19

“Tumekubaliana na wale wanaosimamia mipango ya mazishi kwamba tutagharamia usafirishaji wa miili ya wawili hao na vile vile kujitolea kuisaidia familia kwa namna nyingine ile tutaweza,” Sonko alisema.

Miili ya Kigenda na Mutheu iliopolewa baharini Ijumaa, Oktoba 11, siku 13 baada yao kuzama.

Habari Nyingine: DCI Kinoti ajiandaa kukabiliana na Wairimu mahakamani, amteua Donald Kipkorir kama wakili wake

Nitasafirisha miili ya Mariam Kigenda na Amanda hadi Makueni - Sonko

Mariam Kigenda na mwanawe Amanda walifariki baada ya kutumbukia baharani. Picha: UGC
Source: UGC

Wawili hao walifariki baada ya gari lao kudondoka kutoka kwenye feri aina ya MV Harambee katika kivukio cha Likoni Septemba 29 na kutumbukia mita 58 baharini.

Kulingana na ripoti iliyotolewa mnamo Jumatano Oktoba 16 na mpasuaji mkuu wa maiti wa serikali Johansen Oduor, waathiriwa walifariki kwa kushindwa kupumua.

Kufuatia mkasa huo, Rais Uhuru Kenyatta amempiga kalamu mwenyekiti wa Shirika la Feri Dan Mwazo.

Kupitia notisi ya serikali ya Oktoba 16, Rais Kenyatta aliwafuta kazi mwenyekiti huyo wa KFS pamoja na wanachama Daula Omar, Naima Amir, Philip Ndolo na Rosina Nasigha Mruttu.

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia news@tuko.co.ke au WhatsApp: 0732482690.

administrator

Related Articles