Nusu ya mali ya bilionea Cohen ni yangu, Sarah Wairimu sasa asema ▷ Kenya News

Nusu ya mali ya bilionea Cohen ni yangu, Sarah Wairimu sasa asema ▷ Kenya News

– Urathi wa Cohen ulimpa mjane wake hewa tu

– Wairimu amepinga hilo na kuelekea kwenye mahakama ya juu kutafuta haki

– Wawili hao walikuwa wameoana kisheria na wana kesi mahakamani iliyokuwa ya kutafuta talaka

Mshukiwa wa mauaji ya bilionea Tob Cohen, ambaye pia ni mjane wake, Sarah Wairimu amesema ana haki ya kumiliki nusu ya mali ya bwenyenye huyo.

Kupitia wakili wake Philip Murgor, Wairimu alisema alikuwa ameolewa kisheria na hivyo ana haki ya kurithi mali ya mumewe.

Habari Nyingine: Shule yamulikwa baada ya kudai wanafunzi wanaabudu majini

Nusu ya mali ya bilionea Cohen ni yangu, Sarah Wairimu sasa asema

Mjane wa Tob Cohen aliwachiwa hewa tu kulingana na urathi wa mumewe. Picha: Nation
Source: UGC

Haya yalijiri huku urathi wa bwenyenye huyo ukifunguliwa na kuonyesha kuwa mjane huyo alikuwa mewachiwa hewa tu na Cohen.

Mwendazake alimpa dadake Gabrielle Van Straten jumba lake la kifahari lenye thamani ya KSh 400 milioni, ambalo limekuwa chanzo cha mzozo mkali baina ya Cohen na mkewe.

Vile vile, Gabrielle na nduguye Benard watagawa fedha zake zilizoko kwenye akaunti zake za benki.

Habari Nyingine: Pasta Nga’ng’a kuwazaba makofi waumini wake na habari zingine zilizotamba sana

Wakili Chege Kirundi ambaye aliandika urathi huo wa Cohen, alisema kuwa aliyoyasoma na yale Cohen alitaka licha ya kuwa wakili wa Wairimu tayari amesema kuwa wataelekea kwenye mahakama ya juu kuhusiana na urathi huo.

“Namtakia kila la kheri katika kuukosoa urathi huo kwenye mahakama,” Chege alisema.

Habari Nyingine: Mariga alazimu Raila kurudi chemba ili kupangia Kibra

Nusu ya mali ya bilionea Cohen ni yangu, Sarah Wairimu sasa asema

Mshukiwa wa mauaji ya Tob Cohen Sarah Wairimu. Picha: Standard
Source: UGC

Wakati akiomba mahakama imwachilie mteja wake, wakili Murgor aliiambia mahakama mbele ya jaji Jessie Lessit kuwa Wairimu anafaa kuwachiliwa ili apate nafasi ya kupigania mali yake.

Wakili huyo alikumbusha mahakama kuwa Wairimu pamoja na mwendazake walikuwa na kesi mahakamani wakitafuta talaka na mzozo mkubwa kwenye kesi hiyo ni mali yao.

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia news@tuko.co.ke au WhatsApp: 0732482690.

Subscribe to watch new videos

administrator

Related Articles