Precious Talent: Gavana Sonko atishia kuwatimua wafanyikazi wa kaunti waliofyonza hela za waathiriwa ▷ Kenya News

Precious Talent: Gavana Sonko atishia kuwatimua wafanyikazi wa kaunti waliofyonza hela za waathiriwa ▷ Kenya News

– Sonko alitishia kuwaachisha kazi waziri wa masuala ya Elimu, afisa mkuu wa fedha na afisa wa kusimamia majanga na mikasa

– Alisema watatu hao walimhakikishia familia za wanafunzi waliofariki zilipokea KSh 100,000 kila mmoja

– Jamaa huyo alidai familia za waathiriwa zimehangaika na mazishi ya wanao baada ya kutengwa na kaunti ya Nairobi

– Alisema mchango uliopokelewa ni wa Naibu Rais Ruto pekee

Jamaa wa mmoja wa wanafunzi walioangamia katika mkasa wa shule Precious Talent amezua madai kwamba mchango ambao Gavana wa Nairobi Mike Sonko aliahidi kuwapa haujawafikia.

Kwenye video iliyosambazwa mitandaoni na gavana huyo, jamaa huyo anasikika akisema kuwa familia zilizowapoteza wanao hazijapokea hela zozote kutoka kwa kaunti ya Nairobi.

Habari Nyingine: Likoni: Jamaa ajitupa Bahari Hindi katika kivukio cha feri

Precious Talent: Gavana Sonko atishia kuwatimua wafanyikazi wa kaunti waliofyonza hela za waathiriwa

Gavana Sonko atishia kuwatimua wafanyikazi wa kaunti waliofyonza hela za waathiriwa wa mkasa wa Percious Talent. Picha: Mike Sonko
Source: Facebook

“Serikali ya kaunti ya Nairobi iliahidi kutupa hela wakati wa ibada ya wafu wiki jana, hata serikali kuu yenyewe iliahidi. La kuvunja moyo ni kwamba hatujapokea hela hizo na tumelazimika kujisimamia wenyewe,” jamaa huyo alisema.

Aliongeza kuwa licha ya ahadi hizo zote, ni mchango wa Naibu Rais William Ruto tu umepokelewa huku familia za watoto hao zikipokea KSh 100,000 kila mmoja.

Habari Nyingine: Maafisa wa polisi wakamatwa na bangi

Kwenye ujumbe wake wa Facebook, Soko alitishia kuchukua hatua kali dhidi ya wafanyikazi wake iwapo uchunguzi wake utabainisha madai hayo ni ya kweli.

Naapa kwamba iwapo matamshi ya huyu jamaa ni ya kweli na wala sio siasa za mbunge wa eneo hilo, naona wafanyikazi wa kaunti wakielekea nyumbani,” Sonko alisema.

Alifichua kuwa waziri wa masuala ya Elimu, afisa mkuu wa fedha na afisa wa kusimamia majanga na mikasa walikuwa wamempa ripoti ya kuthibitisha familia zote zilizoathirika zilipokea KSh 100,000 kusimamia mazishi.

Habari Nyingine: Magazeti ya Kenya Alhamisi, Oktoba 3: Ikulu yawaonya wanasiasa kutomtaja Rais wakiwa taabani

Mwanasiasa huyo alisema kuwa serikali ilitenga fedha za kununua masanduku manane ya wanafunzi waliofariki kando na kusimamia usafirishaji wa miili hiyo.

“Watasema hiyo pesa walipeleka wapi. Mimi sichezi na majonzi ya familia zinazoomboleza. Lazima nitimize ahadi yangu na nitafuatilia jambo hilo kesho,” Sonko alionya.

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia news@tuko.co.ke au WhatsApp: 0732482690.

Subscribe to watch new videos

administrator

Related Articles