Raila apate ushindi kwenye chaguzi ndogo, sasa Kibra yasubiriwa ▷ Kenya News

Raila apate ushindi kwenye chaguzi ndogo, sasa Kibra yasubiriwa ▷ Kenya News

– Mgombea wa ODM aliibuka mshindi kwenye uchaguzi mdogo wa Ganda eneo bunge la Kilifi

– Matokeo hayo yatakuwa pigo kwa safari ya kisiasa ya mbunge wa eneo hilo Aisha Jumwa

– Chama cha ODM kimejivunia ushindi huo na kusema ni ishara ya mambo yatakavyokuwa Kibra

Kinara wa ODM Raila Odinga amerekodi ushindi kwenye chaguzi ndogo katika wadi za Ganda na Abakaile Daadab ambapo mashindano makali yalikuwa yametarajiwa kati ya ODM na wapinzani wake.

Katika wadi ya Ganda, ushindani mkali ulishuhudiwa kati ya Reuben Katana wa ODM na Abdulrahman Omar aliyegombea kibinafsi pamoja na Joseph Kiponda wa Jubilee.

Habari Nyingine: Msanii Bamboo afichua jinsi alijiunga na Illuminati kabla ya kuokoka

Raila apate ushindi kwenye chaguzi ndogo, sasa Kibra yasubiriwa

Aisha Jumwa amekuwa muasi wa ODM na kuegemea upande wa Naibu Rais William Ruto. Picha: Aisha Jumwa
Source: UGC

Uchaguzi huo uliwasha joto la kisiasa kwenye eneo bunge la Malindi huku mbunge Aisha Jumwa akijaribu kupambana na chama cha ODM baada ya kuwa muasi.

Jumwa alikamatwa baada ya rabsha kuhusu uchaguzi huo kuzuka nyumbani kwa Katana na kusababisha kifo cha mtu mmoja.

ODM ilijivunia ushindi huo huku wakisema unaashiria mambo yatakavyokuwa kwenye chaguzi zijazo.

Habari Nyingine: Matokeo ya upasuaji wa miili ya Mariam na mwanawe kutolewa na taarifa zingine

Katana alipata kura 4189 huku mpinzani wake wa karibu Omar akiwa na kura 2359.

Uchaguzi huo licha ya kuwa mdogo ulikuwa umegeuzwa na kuwa mashindano ya kisiasa kati ya Raila na William Ruto ambaye anashabikiwa na Aisha Jumwa.

Hayo yanajiri huku uchaguzi wa Kibra ambapo ODM pia wanajizatiti kuibuka washindi wa kiti cha ubunge ukisubiriwa.

Habari Nyingine: Bwana harusi aliyetoweka na kisha kupatikana asema mipango ya harusi bado ipo

Raila apate ushindi kwenye chaguzi ndogo, sasa Kibra yasubiriwa

Mariga ana matumaini kuwa ataibuka mshindi wa kiti cha ubunge cha Kibra. Picha: William Ruto
Source: Facebook

Licha ya wengi wa viongozi kusema kuwa McDonald Maraiga hawezi kushinda kura zozote kwenye uchaguzi mdogo wa Kibra Novemba 7, Naibu Rais William Ruto anaamini mwanasoka huyo ndiye atageuza maisha ya wanaKibra.

Ruto ameahidi kuwa atashinda kiti hicho ambacho kilibaki wazi baada ya kifo cha aliyekuwa mbunge wa ODM Ken Okoth.

Wachanganuzi wa kisiasa wanasubiri kuona iwapo DP atafaulu kuchapa Raila kisiasa.

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia news@tuko.co.ke au WhatsApp: 0732482690.

Subscribe to watch new videos

administrator

Related Articles