Sababu za Sadio Mane kutaka kumlima Moh Salah uwanjani ▷ Kenya News

Sababu za Sadio Mane kutaka kumlima Moh Salah uwanjani ▷ Kenya News

Mohamed Salah alimukaripia Sadio Mane kutaka kujua chanzo chake cha kununa huku akikataa kumpigia pasi mchezaji mwenzake wakati wa mechi ya Liverpool dhidi ya Burnley.

Liverpool walikuwa kifua mbele kwa mabao 3-0 dhidi ya Clarets ugani Turf Moor mwezi Agosti mwaka huu wakati Salah alikataa kumpigia pasi Mane na kisha kutaka kufunga bao.

Habari Nyingine: Paul Pogba na De Gea wabanduliwa katika mechi dhidi ya Liverpool

Moh Salah

Moh Salah alikataa kumpigia mwenzake Sadio Mane na kukimbia kujaribu kufunga bao.
Source: Getty Images

Habari Nyingine: Nyota wa Man City Sergio Aguero ahusika katika ajali akielekea mazoezini

Mzaliwa huyo wa Misri alizuiliwa hata hivyo, nakushindwa kutingisha wavu na kumpelekea Mane kupandwa na mori wakati alipobadilishwa dakika chache baadaye.

Kupitia tuko hilo ambalo iliwapelekea wawili hao kukaribia kulishana makonde kwenye chumba cha kubadilishia, Mane alikuwa na haya ya kusema:

Habari Nyingine: Hatimaye matokeo ya upasuaji wa miili ya Mariam Kighenda na bintiye yatolewa

“Aliniuliza Sadio, mbona umekasirika? Unatakiwa kunipatia mpira, Mo, ambapo alijibu hakuniona. Wajua sina chuki dhida yako. Lakini wajua hisia zake zilikuwa tofauti,” Mane alisimulia Canal Plus

Nyota huyo anasema walisuluhisha swala hilo kupitia njia ya simu na wakapata kurejesha uhusiano wao wa kawaida.

Habari Nyingine: Msanii Bamboo afichua jinsi alijiunga na Illuminati kabla ya kuokoka

“Huwa tunazungumza kwa simu wakati mwingine, huwa tunatumiana ujumbe na hatuna shida. Kwa hivyo tulisuluhisha,”

“Tulisuluhisha sisi wenyewe, na hata kocha aliniita tukazungumza. Nilimwambia tayari tulikuwa tumetatu mzozo wetu,” aliongezea Mane.

Moh Salah

Sadio Mane anasema walisuluhisha swala hilo kupitia njia ya simu.
Source: Twitter

Meneja wa Reds Jurgen Klopp alipuuza kisa hicho baada ya mechi hiyo na kulingana na Mane, hali ilikuwa shwari.

“GeorginioWijnaldum, ambaye anapenda kuwatania watu, alisubiri kila mtu kisha akanijia na kuniuliza kwa sauti ya juu ‘Mo Salah, mbona Mane anataka kukuchapa? kisha kikosi chote kikangua kicheko,” alikumbuka Mane.

administrator

Related Articles