Ugonjwa uliomtafuna Mugabe hadi kummaliza ni saratani, Rais Mnangagwa atangaza ▷ Kenya News

Ugonjwa uliomtafuna Mugabe hadi kummaliza ni saratani, Rais Mnangagwa atangaza ▷ Kenya News

Rais wa zamani wa Zimbabwe Robert Mugabe aliaga dunia kutokana na ugonjwa wa saratani, gazeti la serikali nchini humo limemnukuu Rais Emmerson Mnangagwa.

Kwa mara ya kwanza tangu kutokea kifo hicho, serikali imeeleza kwamba matibabu kutumia miale ya umeme (chemotherapy) aliyokuwa akipewa kupunguza sumu mwilini, yalisitishwa wakati ilipodhihirika kuwa hayasaidii tena.

Habari Nyingine: Babu Owino amjibu Jaguar kuhusu ombi la kutaka amkabili

Kilichomuua Mugabe chafichuliwa na Rais wa Zimbabwe Emmerson Mnangagwa

Mugabe alifariki dunia Ijumaa, Septemba 6 nchini Singapore, akiwa na umri wa miaka tisini na mitano. BusinessLive
Source: UGC

Mugabe alifariki dunia Ijumaa, Septemba 6 nchini Singapore, akiwa na umri wa miaka tisini na tano.

Akizungumza jijini New York anapohudhuria Mkutano Mkuu wa Umoja wa Mataifa wiki hii, Mnangagwa aliwaambia wafuasi wa chama tawala cha Zanu- PF kuwa, Mugabe aliangamizwa na saratani lakini hakutaja ni aina gani kansa hiyo.

Habari Nyingine: Mazishi ya Tob Cohen yaahirishwa ghafla

Kilichomuua Mugabe chafichuliwa na Rais wa Zimbabwe Emmerson Mnangagwa

Rais wa zamani wa Zimbabwe Robert Mugabe aliaga dunia kutokana na ugonjwa wa saratani, gazeti la serikali nchini humo limeripoti. Picha: New Times
Source: UGC

Marehemu anatarajiwa kuzikwa katika eneo la makaburi kunakozikwa mashujaa ambalo linajengwa jijini Harare. Eneo hilo, ndiko kulikozikwa wapiganiaji uhuru wengi nchini humo walio maarufu .

“Matibabu yalisitishwa, madaktari walikatiza matibabu, chemotherapy, moja, kwasababu ya umri wake na pia kwasababu saratani yake ilikuwa imesambaa na matibabu yalikuwa hayasaidii tena,” Mnangagwa alisema na kunukuliwa na gazeti la The Herald, Jumatatu, Septemba 23.

Habari Nyingine: Seneta Cheruiyot ajaribu kupimana nguvu na Matiang’i kwenye mazishi, akiona chuma cha moto

Kilichomuua Mugabe chafichuliwa na Rais wa Zimbabwe Emmerson Mnangagwa

Marehemu anatarajiwa kuzikwa katika eneo la makaburi kunakozikwa mashujaa ambalo linajengwa jijini Harare. Picha: Aljazeera
Source: Facebook

Mnamo mwaka wa 2011, WikiLeaks ilitoa taarifa kuwa Mugabe alikuwa akiugua tezi-kibofu ugonjwa ambao ulikuwa umeenea hadi katika viungo vingine, lakini maafisa wa serikali walikanusha madai ya habari hizo.

Wakati wa utawala wake, rais huyo wa zamani mara kwa mara alisafiri kwenda Singapore kutibiwa, lakini alilazimishwa kung’atuka baada ya mapunduzi yaliyotokea mnamo Novemba 2017.

Mwezi huo, Mugabe aliwekwa kizuizini kwa siku nne huku Mnangagwa akichukua nafasi yake na kuwa kiongozi wa Zanu-PF.

Habari Nyingine: Baada ya fichaficha hatimaye Tanasha athibitisha kumzalia Diamond Platnumz mtoto mvulana

Novemba 21 spika wa bunge la Zimbabwe alitangaza rasmi kujiuzulu kwa Mugabe baada ya muda mrefu kukataa kibabe kufanya uamuzi huo.

Mugabe alifikia makubaliano ya kupata ulinzi kwake na familia yake kutokana na hofu ya kuuawa na kuendeleza biashara yake. Pia alipewa nyumba, wafanyakazi, usafiri na hadhi yake ya kidiplomasia.

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia news@tuko.co.ke au WhatsApp: 0732482690.

Subscribe to watch new videos

administrator

Related Articles