Wabunge wakerwa na mwenzao kutaka kudhibiti WhatsApp, Facebook ▷ Kenya News

Wabunge wakerwa na mwenzao kutaka kudhibiti WhatsApp, Facebook ▷ Kenya News

Wabunge wameudhika baada ya mbunge wa Malava Injendi Malulu kutengeneza mswada unaopania kudhibiti mitandao ya WhatsApp na Facebook.

Kulingana na mswada huo, wote wanaotaka kuanzisha vikundi kupitia WhatsApp am Facebook watalazimika kutafuta leseni kwanza kwa shirika la kudhibiti mawasiliano nchini (CAK).

Habari Nyingine: Sarah Wairimu atoa maneno makali wakati wa mazishi ya mumewe Tob Cohen

Wabunge wakerwa na mwenzao kutaka kudhibiti WhatsApp, Facebook

Mbunge wa Malava Malulu Injendi anataka WhatsApp na Facebook zidhibitiwe. Picha: Malulu Injendi
Source: Facebook

Wakiongozwa na Babu Owino, wabunge walimtaka Malulu kutafuta mswada mwingine kwani bunge haliwezi kujadili mswada wa kiwango hicho.

“Huo ni upuzi. Huwezi kuwanyima vijana uhuru wao wa kuongea kama walivyohakikishiwa kwenye katiba,” Babu alisema.

“Tunafaa kuwa tukishughulika vile vijana wetu watapata kazi, usawa katika ugawaji wa raslimali kuwepo kwa chakula cha kutosha na elimu bora ilhali wabunge wengine wanaleta mchezo tu,” aliongeza.

Habari Nyingine: Seneta Murkomen aelezea sababu za kulia kama mtoto baada ya video yake kusambazwa

Wabunge wakerwa na mwenzao kutaka kudhibiti WhatsApp, Facebook

Mbunge wa Embakasi Mashariki Babu Owino alikerwa na mwenzake kwa kutaka kudhibiti WhatsApp, Facebook. Picha: Babu Owino
Source: UGC

Mbunge wa Dadab Mohamed Dahir alisema Wakenya wanafaa kufanya mageuzi ya kikatiba na kubadilisha viti vya ubunge kwani baadhi ya wabunge hawajui wanalofaa kufanya.

Iwapo mswada wa Malulu utapita, basi wote wanaotaka kuanzisha mitandao ya WhatsApp na Facebook watahitaji watafute leseni za CAK.

Vile vile, iwapo wanaoshiriki michango kwenye mitandao hiyo watafanya kosa lolote, basi itakuwa ni mzigo wa wasimamisi wa vikundi hivyo.

READ ENGLISH VERSION

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia news@tuko.co.ke au WhatsApp: 0732482690.

Subscribe to watch new videos

administrator

Related Articles