Wanasiasa wa Kieleweke washangilia kuanguka kwa Punguza Mzigo ▷ Kenya News

Wanasiasa wa Kieleweke washangilia kuanguka kwa Punguza Mzigo ▷ Kenya News

– Wanasiasa wa Kieleweke wamesema Punguza Mzigo ilikuwa njama ya kuwagawanya Wakenya

– Mswada huo ulikosa kupata uungwaji mkono na kaunti 24 kama inavyotakikana kikatiba

– Kieleweke na ODM walisema wanasubiri mswada wa BBI

Wanasiasa wa Jubilee mrengo wa Kieleweke pamoja na wenzao wa ODM wameshangilia kaunti ambazo ziliangusha mswada wa Punguza Mzigo.

Kwenye kikao na wanahabari Alhamisi, Oktoba 17, wanasiasa hao walisema mswada huo ulikuwa wa kuleta mgawanyiko kwa Wakenya.

Habari Nyingine: Matokeo ya upasuaji wa miili ya Mariam na mwanawe kutolewa na taarifa zingine

Wanasiasa wa Kieleweke washangilia kuanguka kwa Punguza Mzigo

Ekuru Aukot aliongozwa mswada wa Punguza Mzigo. Picha: Standard
Source: Facebook

“Tunataka kupongeza kaunti zote ambazo ziliangusha mswada wa Punguza Mzigo. Isipokuwa kaunti ya Uasin Gishu, kaunti zingine zote zilijadili na kuangusha mswada huo kwa sababu haujumuishi Wakenya wote,” walisema Wabunge hao.

Kundi hilo la wabunge liliongozwa na mbunge wa Nyeri Mjini Ngunjiri Wambugu ambaye alidai kulikua na njama ya baadhi ya viongozi kuwagawanya Wakenya huku taifa likielekea mwaka wa 2022.

“Kulikuwa na wanasiasa ambao walitaka kutumia Punguza Mzigo kama chombo cha kisiasa kuwagawanya Wakenya na pia kuweka vikwazo kwa mswada wa BBI,” alisema.

Habari Nyingine: Wakazi wa Mai Mahiu wahatarisha maisha yao kwa kuchota mafuta baada ya lori kuanguka

Wanasiasa wa Kieleweke washangilia kuanguka kwa Punguza Mzigo

Mbunge Ngunjiri Wambugu amesema Punguza Mzigo ilikuwa njama ya kuwagawanya wakenya. Picha: Ngunjiri Wambugu
Source: UGC

Wabunge hao, wakiwemo Anthony Oluoch wa Mathare, TJ Kajwang’ wa Ruaraka pamoja na mwakilishi wa kina mama kaunti ya Nairobi Gathoni Wamuchomba, walisema wanasubiri mswada wa BBI.

Mswada huo wa Punguza Mzigo haukupata uungwaji mkono na kaunti 24 kama inavyohitajika kikatiba na hivyo itamlazimu Aukot kurudi mezani na kuchora upya.

Habari Nyingine: Siaya: Jamaa abaki kulia baada ya kusahau kubadili noti za 1000 za nusu milioni

Wanasiasa wa Kieleweke washangilia kuanguka kwa Punguza Mzigo

Timu ya BBI ilikamilisha zoezi la kuokota maoni kutoka kwa Wakenya na kwa sasa itatoa mapendekezo yake kwa Rais Uhuru Kenyatta. Picha: Nation
Source: UGC

BBI iliundwa na Rais Uhuru Kenyatta na kinara wa ODM Raila Odinga ili kuchukua maoni kutoka kwa Wakenya kuhusu ni masuala yepi yanafaa kushughulikiwa ili kujenga Kenya.

Baadhi ya juhudi zake ni kuchukua maoni ya kile kinafaa kufanywa kukabiliana na ufisadi, ukabila pamoja na machafuko ya kila wakati wa uchaguzi.

READ ENGLISH VERSION

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia news@tuko.co.ke au WhatsApp: 0732482690.

Subscribe to watch new videos

administrator

Related Articles